SHULE AMABAYO HUFIKIWA KWA NGAZI HUKO CHINA...DAH KUMBE KWA NAMNA HII SIJUI KAMA WANAELEWA WAKIFIKA
Kijiji cha Atuler kimepewa jina la utani "kijiji cha mwamba". Kijiji hiki hupatikana mita 800 juu kwenye nyika eneo la Sichuan, China. Wanaoishi hapa ni watu wa jamii ya Yi, ambao pia hupatikana Vietnam na Thailand
![Kijiji cha Atuler](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_s0rEgu3XGK3k27fydEj0AI1Lq8VOwXCdBm6nzSUQBJVDR2YijlcTW5XTW5m09EzWuUpyT3Q_dcA8KO8CvHSGuUc7w_86gutgipP7DTf_n6fXsFlF12R1WX6NNvxt_4ee8j9GzQfDWFxMLanjmp2oDKpgroUoHxshd_=s0-d)
Hadi kufikia sasa, kulikuwa na ngazi 17 za mbao ambayo ilikuwa njia pekee ya wakazi wa kijiji hiki kutoka nje ya kijiji chao. Kupanda ngazi hizi lilikuwa jambo hatari na watu zaidi ya saba walifariki wakizikwea, wakazi wanasema.
Sasa, ngazi ya chuma imejengwa kurahisisha safari yao. Lakini bado ni shughuli hatari, ingawa muda wanaotumia kupanda na kushuka umepungua
No comments:
Post a Comment